Amesaini mkataba wa kukipiga Azam FC kwa miaka mitatu na kukabidhiwa jezi namba 26. Tukio hilo lilifanyika jana mbele ya meneja wake George Deda.
Highlanders walithibitisha kuondoka na kujiunga na Azam kwa mchezaji huyo. ''Alitutumia meseji akitushukuru kwa kumwachilia aende.'' Alisema Bosso Chief Executive officer Ndumiso Gumede.
''Siku zote nitawakumbuka Bosso na ninawatakia mema msimu huu. Pia nawaomba mashabiki wote waisapoti timu hasa kipindi hiki ambapo mambo sio mazuri sana japo najua ni suala la muda mfupi tu. .'' Alisema Kangwa.
Deda hakuweza kuweka wazi juu ya pesa ilitumika kumnyaka mwanasoka huyo lakini alisema pande zote mbili zimeridhishwa na jinsi mambo yalivyokwenda.
''Ni makubaliano yenye faida kwa pande zote zilizohusika. Bosso wana furaha, Az\m wana furaha na hata Bruce ana furaha. Nataka niwashukuru Highlanders kwa kumwachilia Bruce.''Alisema Deda.
Kangwa anatarajia kuonekana dimbani kwa mara ya kwanza pale watakapopambana na Dar Young Africans katika mpambano wa Ngao ya Hisani ama ''Charity Shield' hapo Agosti 17, 2016 kabla Vodacom League haijaanza kuchanja mbuga hapo Agosti 20, 2016.
Kangwa amekuwa ni mzimbabwe wa nne kukipiga hapa bongo huku wengine wakiwa ni Method Mwanjali, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko wanaokipiga Young Africans.
Je, unadhani Bruce Kangwa ataisaidia Azam FC katika msimu huu kama walivyofanya wenzake wanaokipigia Young Africans?
Comments