Jose Mourinho anajiandaa na game ya Community Shield (official game) akiwa in charge au meneja wa Manchester United katika dimba la Wembley kesho Jumapili.
Timu yake wanaojulikana sana kama Mashetani Wekundu watakutana na mabingwa wa soka Uingereza Leicester City katika mtanange huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwenye wa ngao ya hisani. Na hii itakuwa nafasi ya mwisho kwa wachezaji wa Man United kumwonyesha Jose Mourinho kuwa wapo tayari na mapambano kabla ya ufunguzi wa ligi watakapopambana na Bournemouth weekend ijayo.
Wakati huohuo Mourihno atakuwa anatarajia lile sekeseke la uhamisho kukamilika. Huku Mashetani hao Wekundu wakijiandaa kukamilisha usajili ama uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus ambao utaweka rekodi ya dunia ya kugharimu paundi milioni mia moja.
Inaeleweka kuwa wamekubali dili ya kumrejesha msukuma kabumbu huyo mfaransa mwenye miaka 23 sasa na wakti Mourihno alipoulizwa kama mashabiki watarajie usajili mwingine ndani ya siku chache zijazo alijibu, ''Ndio, sasa tunao 22 na tutakuwa nao 23.''
Msomaji jipange, nitakuletea hayo yote na mechi ya Kombe la Hisani pindi yatakapojiri. Cheers!
Comments