SIMBA SC wametupilia mbali madai kuwa wameahirisha Simba Day bonanza, litakalofanyika Jumatatu jijini Dar es Salaam, kufuatia kutiwa nguvuni kwa kiongozi wa club hiyo na Taasisi ya kupambana na kuzuia rusha ''Prevention and Combatting of Corruption Bureau (PCCB).''
Haji Manara, mkuu wa Habari Simba SC
Mwana habari mkuu wa club, Haji Manara alisema jana Dar es Salaam kuwa annual bonanza, ambayo kwa mwaka huu itaenda pamoja na sherehe za club ya Simba kutimiza umri wa miaka 80 tanga kuanzishwa kwake litafanyika kama ilivyopangwa katika uwanja wa taifa Dar.
Simba ilianzishwa mwaka 1936 na sasa wamepanga kitu tofauti kwa sherehe hizo za kumbukumbu kwenye hiyo 'Simba Week' ambapo wanachama, wachezaji na viongozi watahusika katika michezo na mambo mbalimbali.
Walakini habari zilizuka kuwa tukio hilo limeahirishwa kufwatia kutiwa nguvuni kwa Rais wa timu ya Simba Evance Aveva na PCCB, mbali na Aveva, wajumbe wengine wanasemekana kuhojiwa na PCCB kuhusiana na suala hilo ambalo rais wao anashtakiwa kwa kosa linalohusishwa na rushwa.
Manara alisema kwamba kila kitu kipo sawa wakisubiri kwa hamu tukio la Bonanza kuanza, akiwaomba mashabiki wa Simba waje kwa wingi uwanjani kushuhudia tukio hilo ambalo alidai litakuwa ni la aina yake.
Kuthibitisha kuwa hakuna kilichobadilika pamoja na kilichotokea, Manara alisema kuwa viongozi na wanachama wa timu watasafisha maeneo yazungukayo Msimbazi Street mahali ambako ni makao makuu ya club. Mbunhe wa Ilala Mussa Azzan Zungu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shughuli yao hiyo.
Nini maoni yako!?
Comments