Jose Mourinho amedokeza kuwa uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Manchester United uko karibu kukamilika.
Akiongea kuelekea mpambano wa Community Shield dhidi ya Leicester City, manager wa United amethibitisha kuwa alikuwa akitarajia mchezaji mwingine zaidi kuwasili Old Trafford kabla ya Agosti 14.
Ingawaje alisema hapendeleai kuongelea habari za wachezaji wa timu nyingine, lakini alisema amepungukiwa na mchezaji mmoja kwani timu yake ya kwanza yaani first squad anataka iwe na wachezaji 23 jumlisha makipa watatu. "We have 22 and we are going to have 23," Mourinho told a news conference. "We are going to get a very good midfielder," he added.
"Paul Pogba ni mchezaji wa Juventus hadi pale atakapokoma kuwa hivyo rasmi, hivyo tunabaki hivyo.'' Alisema Mourihno.
Mourinho alisema pia kuwa anatarajia kuutumia mchezo wa Jumapili kutoa nafasi ya kutosha kwa wachezaji wake. s
"Tunaweza kufanya mabadiliko ya wachezaji mara sita badala ya tatu, hivyo hiyo inatoa muda kwao.'' Alisema.
"Pia inanipa nafasi ya kuchezesha wachezaji ambao najua hawawezi kucheza dakika 90, kwani hawawezi kucheza dakika 90. Na tutajaribu kushinda mechi hiyo.''
Leicester manager Claudio Ranieri apia alisema anatarajia mchezo kuwa wa ushindani. l
"Tutatoa ushindani wa kutosha kama wao ''Manchester United'', itakuwa ni mechi ya nguvu sana.'' Alisema Ranieri ambaye itakuwa ni mara yake ya kwanza kama manager katika uwanja wa Wembley.
Comments