Jose Mourinho amekubali kuwa itachukua muda kidogo kwa Manchester United kubadilisha style ya uchezaji toka ile ya Louis Van Gaal kwenda ile ya kwake.
Mourinho ametwaa kikosi hicho kama boss au manager mwezi Mei mwaka huu kama mrithi wa Van Gaal, ambao walicheza style ambayo ilikosolewa sana kuwa haikuvutia.
Alipoulizwa kuelekea pambano la Community Shield siku ya Jumapili dhidi ya Leicester City kuhusu mabadiliko ya kiuchezaji ya wachezaji wa United, Mourihno alikuwa makini na kusema kuwa filosofia yake ni tofauti na ile ya Gaal.
Je ni kweli kwamba itachukua muda kwa manchester united kubadilika style ya soka?
Comments