Fifa World Cup 2018. Mechi za Kwanza. Ronaldo Acheka, Messi Anuna Tuziangalie mechi za ufunguzi, yaani mechi za kwanza kwa kika timu ama nchi kwenye mashindano ya fainali za kombe la dunia 2018 kule Urusi lakini hasa kwa mataifa mawili wanayotokea mastaa ama wapinzani wakubwa wawili ambao wanacheza kwenye La Liga kule Hispania, namaanisha Mreno Cristiano Ronaldo na Muajentina Lionel Messi. Katika mechi yao Ureno ama Portugal vs Spain, Ronaldo aliibuka shujaa baada ya yeye na wenzake kulazimishana droo ya 3-3 dhidi ya Hispania huku Ronaldo akiweka rekodi nyingine, akifunga hat trick yaani mabao matatu ndani ya mechi moja, kwa penati, shutu la mbali pamoja na free kick. Ronaldo akishangilia goli Kwa upande wa hasimu wake mkubwa Lionel Messi, yeye leo ameshindwa kabisa kufurukuta wakati taifa lake Argentina walipovaana na Iceland. Akipiga mashuti 11 hakufanikiwa kabisa kutikisa nyavu za Iceland kwani hata goli lao lilifungwa na Aguero. Huku akipata nafasi sawa na Ronaldo, yaani...
Comments