Skip to main content

Tha ''Battle'' Of FA CUP Chelsea vs Man United

Ukiangalia kwa haraka haraka unaweza kutoa matokeo ya mechi hii hata kabla haijachezwa na wala hakuna mtu atakaekushangaa kwa huo ndio mtazamo wa mashabiki wengi wa soka na hata wataalam wa uchambuzi wa kimataifa wa soka. Kwanza Manchester United alichezea kichapo cha magoli 4-0 pale Darajani wakati wa mechi yao ya Premier League dhidi ya Chelsea, mechi ambayo kwa mujibu wa Jose Mourinho ni kwamba 'ilianza na goli' hivyo hakujua nani wa kumlaumu. Leo Man United na Mourihno wanarudi tena Darajani katika robo fainali hii ya FA cup wakiwa na kumbukumbu zile zile za kichapo.

Kwa matazamo mwingine ukiiangalia Manchester United utagundua sio ile iliyopigwa 4=0 na Chelsea kwa maana kwamba imebadilika kwa kiasi kikubwa wakiwa na ari, nguvu na determination ya ushindi, huku wakiwa wamecheza mechi nyingi zaidi bila kupoteza katika mashindano mbalimbali ya ndani na ya nje.

Lakini je, Manchester United wakiwa ndio mabingwa watetezi wa kombe hili la FA watakubali kuupoteza mchezo huu muhimu kwao hata kama wanakutana na Chelsea ambao wanaonekana kuwa na nguvu zaidi yao. Lakini pia je, Chelsea wao wapo tayari kweli kuupoteza mchezo huu na hatimae wayaage mashindano haya kwa kufungwa na Man United? Hayo ni maswali tu ambayo unapaswa kujiuliza na nina uhakika majibu utakayojipatia yatakuchanganya hata wewe mwenyewe kwani mechi hii inatarajiwa kuwa ngumu na inayofananishwa na fainali.

Mourihno, meneja wa Manchester United akidai kuwa kuna uwezekano Chelsea wakacheza mchezo wa kujilinda zaidi kitu ambacho kinapingwa na Konte, meneja wa Chelsea.

Mourinho akimzungumzia Rashford

"Ni maamuzi yake mwenyewe. Anajua kuwa ndiye mshambuliaji pekee mwenye nafasi kubwa ya kucheza na hawezi kukwepa hilo'' 

VIKOSI
CHELSEA
Courtois; Azpilicueta, Luiz, Cahill; Moses, Kante,  Matic, Alonso; Willian, Costa, Hazard.
Substitutes Begovic, Fabregas,  Zouma, Pedro, Batshuayi, Terry, Chalobah. 

MAN UNITED
De Gea; Jones, Smalling, Rojo; Valencia,  Ander Herrera, Pogba, Darmian; Mkhitaryan, Rashford, Young.
Substitutes Romero,  Bailly, Mata, Lingard, Carrick, Blind, Romero, Fellaini.

 Referee Michael Oliver (Northumberland)

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...