Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2017

Zoezi la kutoa dawa za minyoo na kichocho lafanyika jijini Arusha

Katika harakati za kutokomeza matatizo ya minyoo na magonjwa ya kichocho serikali imetoa chanjo jijini Arusha Jana kwenye mashule mbalimbali likiwa ni zoezi la kitaifa ambalo linaenda kwa awamu kadhaa. Jana nilifanikiwa kushuhudia zoezi hilo likifanyika katika shule ya Highridge iliyopo maeneo ya Njiro/PPF karibu na General tyre. Utoaji huo wa dawa hizo ulikuwa ni kwa wanafunzi wa kuanzia shule ya awali hadi darasa la saba. Nikiongea na mwalimu Alia John wa Highridge kuhusu changamoto ya zoezi hilo alisema, "Kuna baadhi ya watoto wachache sana walitapika baada ya kupewa dawa hizo, na wazazi wachache kukosa imani na dawa hizo na kujaribu kuzui watoto wao wasipewe lakini mara baada ya kupewa elimu walikubaliana na zoezi hilo kufanyika kwa watoto wao." Alisema mwalimu Alia John ambaye alikuwa mmojawapo wa maofisa walioshiriki katika zoezi hilo.

EPL na BUNDESLIGA jana