Skip to main content

Aliyoyanena Zitto Zuberi Kabwe kuhusu kusitishwa kwa misaada

Tupeane maarifa tu kidogo. Duniani kote Nchi inapokatiwa Misaada watawala hutumia fursa hiyo kujenga hoja za kizalendo kuwa hatuendelei kwa sababu tumekatiwa misaada. Zimbabwe ni mfano mzuri sana juu ya jambo hili. Burundi ndio hali inayoendelea hivi sasa.

Hapa Tanzania hali ya Uchumi ni mbaya sana, mbaya mno. Uzalishaji umeshuka, kote mashambani na viwandani. Uzalishaji kwenye kilimo umeshuka mpaka kufikia 0.6% kwa mwaka kutoka 2.5% kwa mwaka, Uzalishaji Viwandani umeshuka kwa karibu 50%. Mapato ya wananchi yameshuka sana. Hivyo kila mwananchi anajua kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kabisa kuendesha uchumi wa nchi.

Kutaka misaada ikatwe ni kuwapa watawala hawa kisingizio cha kushindwa kuendesha Uchumi kwa sababu ya sera mbaya. Misaada ikikatwa Watawala watasema "hatuendelei Kwa sababu tumekatiwa misaada, kwa sababu ya vita ya kiuchumi (msamiati wa kimkakati ambao washaanza kuutumia)", wakati hali halisi ni kuwa wameshindwa kuendesha Uchumi.

Kwanini muwape watawala visingizio wakati uchumi huu utaanguka tu kwa uendeshaji mbaya? Kiongozi yeyote mwenye akili timamu na mwenye kutazama mambo kimkakati hawezi kutaka misaada ikatwe bali atawaeleza wananchi kuwa uchumi unaporomoka kwa sababu ya sera mbaya na kwa sababu watu hawana Uhuru na demokrasia, maana uhuru wa demokrasia huleta mezani mawazo, sera na mbinu mbadala za kuendesha uchumi, tofauti na hali ilivyo sasa.

Hatupaswi kamwe kuingiza wageni kwenye  jambo hili. Tunaliweza wenyewe.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Kigoma
Julai 20, 2017

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...