Arsenal Washinda Ngao ya Hisani (Community Shield) FT: Arsenal 1-1 Chelsea. Penalties: Arsenal 4-1 Chelsea. Na matukio mengi katika picha.
Hatimaye Mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ya Ngao ya Hisani kati ya Arsenal dhidi ya wenzao wa jiji la London Chelsea imepigwa na kukamilika kwa Arsenal kutwaa Ngao ya Hisani baada ya kuwabanjua mabingwa wa Epl 2016-2017 Chelsea kwa penati 4-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika 90.
Katika mchezo huo uliokuwa safi, wenye ushindani na uliotawaliwa na faulo za hapa na pale ulishuhudiwa mshambuliaji wa Chelsea Pedro akizawadiwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya na kuwafanya vinara Hao wa Epl kutoka jiji la London kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu. Kadi za njano pia zilikuwa za kutosha kutokana na mchezo mbaya waliokuwa wakichezeana pande zote mbili.
Comments