Skip to main content

DAR: PAUL MAKONDA AZUIA AGIZO LA KUONDOA VIOO VYENYE TINT KWENYE MAGARI

HIVI PUNDE :
PAUL MAKONDA AZUIA AGIZO LA KUONDOA TINT KWENYE MAGARI

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amewaagiza Polisi jijini Dar kusitisha utekelezaji wa amri inayowataka wananchi wenye magari kuondoa tint kwenye vioo vya magari yao.

Agizo hili ambalo hapo awali utekelezaji wake ilikuwa uanze kesho, Paul Makonda amesema litawaletea usumbufu wananchi kwani sababu za utekelezaji wake hazina mashiko.

"Tafsiri yake ya kwanza ambayo agizo hilo inapeleka kwenye jamii ni kuwa wenye tinted kwenye vioo vya magari yao, kama sio wao basi wanaoyatumia, ni wahalifu. Jambo ambalo si kweli kwani yapo magari yanakuja yakiwa na vioo tinted, pia wengine wanaitumia tinted kama njia ya kujilinda dhidi ya watu wabaya hasa wakinamama," amesema Paul Makonda.

"Aidha, mkoa wa Dar Es Salaam sio kisiwa, kuna watu wanaingia kila siku; Je, magari yao tu nataka wayapaki Chalinze?" ameuliza kwa mshangao Paul Makonda.

Paul Makonda amehitimisha kwa kuwataka Polisi kutafuta njia sahihi ya kupambana na wahalifu badala ya kutumia zinazoweza kuleta usumbufu kwa wananchi.

Source: #Dar24

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...