Goli lilipigwa na super sub Anthony Martial lilitosha jana kuipa Manchester United ushindi katika dimba la nyumbani Old Trafford na kuwanyamazisha kabisa Totten Ham Spurs na mashabiki wao.
Spurs wako kwenyw form ya hali ya juu na inashikilia nafasi ya tatu kwenye masimamo wa ligi hiyo ya EPL nyuma ya United na vinara wakiwa ni Manchester City.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, timu zote mbili zilicheza vizuri na kuwa na kosakosa za hapa na pale hasa Man United ambao walionekana wenye ari ya ushindi hasa ikizingatiwa walikuwa nyumbani.
Wengi walitarajia kwamba United wangepaki basi kama walivyofanya nyumbani kwa Liverpool ama kupoteza mchezo huo kama ilivyotokea nyumbani kwa Huddersfield, lakini matarajio yao hayo yaliyoyoma na kushuhudia Manager wa United José Mourihno akimtoa Marcus Rashford na kumwingiza Anthony Martial ambaye baada ya muda alipokea pande toka kwa Romelu Lukaku aliyempasia kwa kichwa (assist) naye bila ajizi aliwatoka mabeki wa Spurs na kuupeleka mpira kushoto kwa kipa wa Spurs na kuandika bao pekee na la ushindi kwa Manchester United ambao wamefikisha pointi 23 wakiwazidi Spurs kwa point 3 na kuendelea kushikilia nafasi ya 2 nyuma ya vinara Manchester City.
Katika mchezo huo ulishuhudiwa makocha wa pande zote mbili wakiwa watulivu wakitoa maelekezo ya hapa na pale kwa wachezaji wao. Na wakati wa half time wakielekea vyumbani, Mourihno akionekana akiwaambia mashabiki wa United watulie kwani nafasi ushindi bado ilikuwepo. Mashabiki hao walionekana kutotulia na kutaka kumlaumu manager wao kwa nini hakuna ushindi au kwa nini timu inachelewa kufunga goli.
Ngome ya United ilionekana kuwa imara ikiongozwa na Eric Bailly, Smalling, Valencia na Jones, walicheza kwa utulivu na mawasiliano ya hali ya juu kuhakikisha ushindi unapatikana bila kuruhusu goli yaani clean shit wazungu wanasema.
Katika mechi nyingine za Premier League ilishuhudiwa Arsenal wakiwanyuka Swansea City 2-1, Chelsea wakipata ushindi wa 1-0 na Man City wakiwafunga West Brom 3-2. Crystal Palace wakitoka sare ya 1-1 na West Ham, huku Watford wakinyukwa 1-0 na Stoke City.
Comments