Skip to main content

Aliyoyaandika Mh Lazaro Nyalandu katika ukurasa wake wa Facebook baada ya Kigwangala kumtuhumu Bungeni

INASIKITISHA sana kuona WAZIRI Kigwangalla akitumia MUDA wake ndani ya BUNGE leo kunichafua, kunidhihaki, na kusema UONGO na UZUSHI dhidi yangu, ikiwa ni NJAMA za makusudi zilizopangwa kunichafua mara baada ya mimi kukihama Chama Cha Mapinduzi -CCM. Aidha, hatua hiyo imepangwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi yeyote wa CCM atakayethubutu ama kudiriki tena kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM katika Serikali hii ya awali ya tano. AIDHA, Waziri Kigwangalla anatumika VIBAYA, kwa u za UONGO na UZUSHI aliuanza DHIDI yangu mara tu alipoteuliwa, kwa kuanza kutoa kauli za kejeli dhidi ya UTUMISHI wangu uliotukuka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na wenye REKODI thabiti.

NIANZE na UZUSHI alioutoa Waziri Kigwangalla  mapema leo BUNGENI, huku moyoni mwake akiwa anajua fika kuwa ametumwa kusema UONGO dhidi ya Waziri Nyalandu kwa lengo la kuandaa MAZINGIRA ya kumkamata na kubwa zaidi, kudhalilisha azma ya WATANZANIA ambao WAKO tayari kwa mabadiliko ya UONGOZI wa nchi kupitia UPINZANI. AIDHA, propaganda za Kigwangalla ameamua zimuhusu Waziri moja tu wa Maliasili, Lazaro Nyalandu, jambo linalothibitisha NJAMA na Progaganda za kuzimisha MOTO na nguvu ya umma kupitia UPINZANI, hasa baada ya kitendo changu Cha kukihama CCM.

1) WAZIRI Kigwangalla amekejeli kuwa Waziri Nyalandu alitumia Fedha za Serikali kusafiri USA na mwanadada Aunt Ezekiel.
-HABARI hii ilikuwa ya KUZUSHA na ilichunguzwa na vyombo vya dola 2014 na kuthibitika ilitungwa na ilikuwa ya UONGO. Katika Mkutano huo wa Washington, DC, Waziri Nyalandu alialikwa na Balozi wa Tanzania, Marekani, na alipewa RUHUSA ya maandishi na Serikali kuhutubia Mkutano huo kwa siku Moja. Wasanii wote
Walioalikwa, akiwepo Mwanadada Aunt Ezekiel, hawakuwa na mwaliko wa Wizara ama Serikali, bali waandaji wa Kongamano. Na Serikali haikulipa gharama zozote kwao.(Mthibiti
Na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anaweza kuthibitisha)

2) Waziri Kigwangalla amedanganya BUNGE kuwa Waziri Nyalandu alitumia helikopta kugombea URAIS 2015.
-Habari hii ni ya uzushi na UONGO, na Waziri atakuwa aidha hana BUSARA ambayo angepaswa kujiridhisha na Taarifa kabla ya kuisoma Bungeni, ama waliomtuma wamemwambia ASOME TU hivyo hivyo. UKWELI ni kuwa, Waziri Nyalandu, alipokuwa CCM, aligombea katika kinyang’anyiro cha URAIS kuomba kuteuliwa ndani ya CCM, na alitumia aidha usafiri wa MAGARI au NDEGE za kawaida kwa kulipa nauli (fixed wings pale ilipobidi), hadi mchakato ulipoisha kama uilivyoisha.
-AIDHA, miaka yote nikiwa Mbunge wa CCM Singida Kaskazini, nimekuwa nikifanya kampeni za kumalizia kwa njia ya helikopta na sijawahi kupata karipio lolote, tangu  Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2000, 2005, 2010, na 2015.
-AIDHA, Mwaka 2015 nilitumia Helicopter kwa SIKU TATU za kumalizia Kampeni, na nilikodi helikopta hiyo kwa Sh milioni tano kwa siku (Jumla, milioni 15)
-Pia ingependeza kama hamaki za Kigwangalla zingemkumbusha kuwa Waziri Nyalandu akiwa Wizarani ALIPATIA Serikali Helikopta mpya Moja, alileta ndege kwa matumizi ya kupambana na Ujangili, Alishawishi Benki ya dunia, Ujerumani na USA kuleta mamilioni ya dola za kmarekani kusaidia mapambano hayo, na kwamba alifanikiwa Sana kutokmeza ujangili nchini. RAIS KIKWETE alikiri hili wakati wa kuzindua Tangazo la Tanzania (Tanzania, the soul of Africa).

3) Kigwangalla amezusha kuwa Waziri Nyalandu alitumia vibaya madaraka yake. Amezungumzia suala la Waziri Nyalandu kutotia sahihi TOZO mpya zilizopendekezwa na TANAPA. Jambo ambalo Waziri Kigwangalla  angepaswa kulijua kabla ya kutoa kauli isiyo sahihi Bungeni ni kuwa SAKATA la TOZO za Tanapa lilijadiliwa BUNGENI mbele ya Spika Mama Anne Makinda, likiwa limeletwa na Kamati ya Lembeli, na kwa kupitia Wizara, Waziri Nyalandu alilitolea ufafanuzi na likamalizika na GN ilitolewa.
-SAKATA la kupandishwa ghafla kwa TOZO za mahotelini zinazojulikana kama (Fixed Rates) lilianza kabla sijawa Waziri. Aidha, kulikuwa na kesi Mahakama Kuu, ambako hadi kufikia mwaka 2012, uamuzi wa Mahakama uliyotolewa. Bado Nyalandu hakuwa Waziri. Aidha, nilipoteuliwa kama Waziri, Nikatazama SAKATA hilo ambalo lilishachukua muda mrefu sana hadi kufikia 2014, mimi nilipokuwa Waziri. Sheria inasema ”Concession Fees shall be 10% of half Board”, na kulikuwa
Na GN ya Serikali kuhusu TOZO hizo, takribani kuanzia mwaka 2002. Hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu ilielekeza kuwa TOZO zozote mpya ni sharti zipate GN mpya, na sheria ya msingi ilitaka TOZO ziwe kwa asilimia (percentage),  na sio TOZO za kukisia, (fixed rate) ambazo ndio msingi mkubwa wa kupendeleana na rushwa katika kupanga nani alipe kiwango gani Cha kodi. Baada ya kuitolea maelezo Bungeni (na hansardi Zipo), Bunge na Wizara tulikubaliana namna ya kulimaliza Sakata hilo,  na ndivyo ilivyofanyika na GN ilitolewa., na nilifuata matakwa ya sheria na Kanuni. Waziri Kigwangalla hajasema ukweli na amezusha kuhusu suala hili kwa sababu anazozijua mwenyewe.

4) Sakata la VITALU: Inasikitisha SANA na inatia AIBU kwamba Waziri atalihadaa BUNGE kwamba Waziri Nyalandu amehusika na kuuza VITALU au kugawa VITALU, na baya Zaidi kwa NJIA ya RUSHWA.
-Sheria ya Wanyamapori inatamka wazi kuwa VITALU vitagawiwa kwa wawindaji kwa kila baada ya miaka MITANO.
-Mara ya mwisho VITALU vimegawiwa Januari, 2017. Nyalandu hakuwa WAZIRI. (Waziri alikuwa Mh. Prof Maghembe)
-Kabla ya hapo, VITALU viligawiwa mwaka 2013. Nyalandu hakuwa Waziri. (Waziri alikuwa Mh Maige)
Hii ni AIBU sana na natumaini kwa Waziri Kigwangalla na wanaomtuma wangetamani sana miaka ibadilike ili isomeke Waziri Nyalandu.

5) Waziri Kigwangalla amedai kuwa Waziri Nyalandu alikuwa anafanyia Kazi katika Chumba maalumu katika hoteli ya Serena.  Naomba Waziri Kigwangalla, athibitishe ni Chumba namba ngapi, na wahusika wa hoteli pia wathibitishe. Kama Waziri, nilifanya Kazi katika ofisi yangu iliyopo Wizaranya Maliasili na Utalii. Kigwangalla pia akumbuke mimi nilikuwa MTEULE wa Rais ambaye alikuwa na vyombo vya kumsaidia kusimamia Mawaziri.

6) MADAI kwamba Nyalandu alihusika na Sakata la kusafirisha TWIGA NJE ya nchi mwaka 2011/2012 ni UZUSHI na UONGO  zaidi ya ule asemao Shetani Ibilisi mwenyewe na siwezi kukaa kimya! Mwaka 2011/2012 nilikuwa NAIBU WAZIRI wa VIWANDA na BIASHARA. Unanihusishaje na Yaliyotokea au kutuhumiwa Wizara ya Maliasili? Uongo huu ni wa aibu na ni kazi ya Shetani Lucifa mwenyewe, na MUNGU wa Mbinguni awakemee wote wanaohusika.

7) Mbwembwe hizi na kusingiziwa kunakofanywa kwa makusudi baada ya mimi Nyalandu kukihama CCM ni aibu kwa TAIFA na ni matumizi mabaya sana ya MADARAKA. Aidha, ifahamike kuwa Vitisho na njama dhidi yangu na familia yangu kunakofanywa na wote wanaohusika hakutazuia azma ya watanzania kutaka mabadiliko ya kweli nchini. Imeandikwa, WAONGO wote, sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto kwa kiberiki. Haki huinua Taifa, na uonevu na dhuluma ni dhambi itakayowatafuna wahusika siku zote za Maisha .

—� —�—� —�—
Lazaro S. Nyalandu

Comments

Popular posts from this blog

Britney Spears' Busy Vegas Weekend With New Beau. Via abc News

Britney Spears keeps it busy in Sin City. The "Scream & Shout" singer spent last weekend in Las Vegas but she wouldn't have come at all if her much-discussed Vegas residency was not a "done deal," the Las Vegas Sun reported. With new boyfriend David Lucado in tow, Spears flew to Vegas Friday and checked into Caesars Palace, the Sun reported. She attended a charity Cirque du Soleil performance, sneaking in just as the curtain went up and leaving just before the show ended. Spearstweeted a photo of herself, Lucado and her manager, Larry Rudolph, smiling in their seats together. Spears' management and production team met with executives at Caesars Entertainment Saturday, which owns Planet Hollywood, and then checked out the PH Live theater, where Brit will have her residency. Spears, Lucado and her entourage then lunched at the Meatball Spot restaurant, owned by Top Chef Seattle contestant Carla Pellegrino. The couple chowed down on meatball s...

Read What Shakira Says. Via Yahoo!

Looking at  Shakira  and her fabulous figure you might be surprised to learn it was only three months ago that she gave birth to son Milan. But the “Hips Don’t Lie” singer reveals that dropping the pounds was no cake walk. While promoting “The Voice” in Pasadena, California, on Monday, the blond bombshell revealed, "[Losing baby weight] is the only thing that’s been a little stressful … I knew I had to come back here to do ‘The Voice’ two months after I had delivered a baby. I didn’t have my four months of maternity like every woman on Earth has. I’m not trying to complain, but it’s been a process full of challenges.” Photo source: omg INSIDER & Yahoo The 36-year-old mama added that the pressure to shed the baby weight at record speed is something that she feels the previous generations didn't face. She said, “I think that our mothers and grandmothers weren’t under the pressure women of today are after delivering a baby. My dad says there’s nothing better than meat...

Jones With A Knee Surgery

Bleacher Report Writes: Manchester United defender Phil Jones is facing up to eight weeks on the sidelines after having surgery on a knee injury, the club has announced.   Jones, 20, has yet to make an appearance this season after hurting his back during pre-season and suffered this latest injury in training. "Phil Jones has had surgery on a knee meniscus tear sustained in training," said a United spokesman. "It will require six to eight weeks of rehabilitation." Jones, whose last competitive appearance for United was against Sunderland on the final day of last season, is understood to have suffered his latest injury in training earlier this week. The England international was sent for a scan on his right knee which has confirmed he requires an extensive period of rehabilitation. Jones was believed to be close to returning following back spasms when he damaged his knee. ...