Zikiwa zimepita siku tatu tu tangu David Kafulila ahame CHADEMA, Leo amekabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama wa CCM na Humphrey Polepole wakati wa kampeni za udiwani kata ya Mbweni jijini Dar es Salaam.
Bwana David Kafulila alitangaza rasmi kuhama CHADEMA siku ya Jumatano kwa madai kwamba upinzani hauna nia ya kupambana dhidi ya ufisadi.
Kitendo cha Kafulila kuhama CHADEMA kumeleta gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa siasa nchini huku swala hilo likienda mbali zaidi na kugusa hata yao hasa pale ilipofahamika kwa mume amehamia CCM na kumwacha Mke CHADEMA akiwa mbunge wa viti maalumu. Kituko zaidi ni pale Mke aliposikika akidai kuwa mume wake atoe Sababu za msingi za kuhama chama na kwamba hakumshirikisha maamuzi hayo. Naye Kafulila alisikika akidai kuwa swala la yeye kuhama chama halina mahusiano yoyote na ndoa yake.
Comments