Akiwa katika kampeni za Kumnadi mgombea wa udiwani kata ya Makabi wilayani Meru, waziri mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa alijibu hija zilizokuwa zikienea kwamba ana mpango wa kurudi CCM. Amesema kuwa taarifa zozote zinazodai hivyo ni za uzushi na zina lengo la kupotosha.
Muungwana Blog iliandika kuwa kuna habari zilizoenea kuwa Mrisho Gambo amepokea ujumbe toka kwa mzee wa Monduli uliomtaka kuzungumza na Rais na kama atakubali basi mzee huyo atarejea nyumbani. Lakini mzee Lowassa amezikana habari hizo na kusema kuwa ni upotoshaji na kwamba yeye hana nia wala ndoto za kurejea CCM.
Comments