MANGE AMTAKA MKE WA DAVID KAFULILA KUOMBA TALAKA
Mange Kimambi ameibuka na kumtaka mke wa mwanasiasa maarufu nchini David Kafulila kudai talaka kwa sababu ya kitendo cha mumewe kuhama chama cha CHADEMA.
Kwa mujibu wa mke wa Kafulila, mumewe alihama chama bila kumshirikisha kama mke wake na kuwa sababu alizozitaja za kumfanya ahame hazina mashing. Hivyo Mange Kimambi amemwomba kama kweli yuko serious na hilo basi adai talaka ama la itakuwa ni mambo ambayo wameshirikiana kupanga ili wale kotekote. Yaani mke apate mshiko CHADEMA ambako yeye ni mbunge wa viti maalum kupitia chama hicho kinara cha upinzani na mumewe ale CCM alikohamia.
Pia Mange aliendelea na swaga hilo kwa kumshauri kuwa pindi atakapodai talaka asisahau na kudai matunzo ya mtoto wazungu wanaita "child support" Kwani mumewe kwa sasa ana hela kinyama. Na kwamba yeye bado ni mrembo hatakosa mtu. Hehe he.
Mh haya bhana. Msomaji sijui imekaaje hii mtu wangu wa nguvu? 👀👀
Comments