Wakicheza Katika performance ya juu ya umiliki wa mpira ukiwa 74% kwa 26%, 70% kwa 30% na 72% kwa 28%, Manchester United walishindwa Kabisa kuchungulia nyavu za Basel Katika mchezo wa ligi ya Mabingwa ama champions League ya ulaya. Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Basel 0, Manchester United 0. Lakini mambo yakabadilika kwenye kipindi cha pili katika dakika ya 89 pale mid field ilipozubaa kidogo na kusababisha Michael Lang kupokea krosi aliyoizamisha nyavuni na kumwacha kipa Romero asijue cha kufanya.
Bado Manchester United wanashikilia usukani katika kundi lao wakiwa na pointi12 ambazo zinaweza kufikiwa na CSKA Moskva endapo watawafunga Manchester United magoli kuanzia 7 pale watakapokutana kwenye mechi yao ya mwisho ya kundi lao ili waweze kuibuka vinara wa kundi hilo
Comments