Zipo fununu kuwa meneja wa Manchester United anataka kuimarisha kikosi chake kwenye safu ya ushambuliaji kwa kumwinda striker kutoka Atletico Madrid ya Uhispania.
Mitandao mbalimbali ulaya imeanza kuandika fununu za uhamisho maarufu kama usajili wa dirisha dogo la Januari huku anayetajwa sana kujiunga na United si mwingine bali Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.
Akihojiwa juu ya tetesi hizo mwenyewe Griezmann amesema kuwa bado ana mkataba mrefu na timu yake ya Atletico Madrid lakini hilo haliwezi pia kumzuia kuondoka huku akidai anataka kumalizia soka lake Marekani kama alivyofanya David Beckham ambaye alikuwa akimtukuza sana.
Griezmann aliendelea kusema kuwa uwezekano wa kutimkia Uingereza hasa Manchester United upo isipokuwa kikwazo kikubwa ni hali ya hewa ya huko.
Je, Manchester United watafanikiwa kusajili Griezmann kwenye kipindi cha usajili wa dirisha dogo hapo Januari 2018?
Comments