Skip to main content

#EPL. MANCHESTER UNITED 2, CHELSEA 1.

MANCHESTER UNITED 2, CHELSEA 1
Willian kwa Chelsea,  Lukaku na Lingard kwa Man United. Man of the match:  Romelu Lukaku,  one goal and one assist.

#AbelRKayUpadates

Vyombo vingi vya habari katika uchambuzi wao juu ya mechi hii viliipa Chelsea dalili kubwa ya kushinda game hii wakati vingine vikitoa uchambuzi wenye kuleta utata lakini ukifwatilia vilionesha kui favor the blues.
Lakini nilipofwatilia mitandao ya kubeti ilionesha Manchester United kuizidi Chelsea kwa pointi kidogo, sasa sijui kama walikuwa wanajaribu kuwa deceive watu ili wapoteze bet zao. Hilo wanalijua wao.

Nijualo mimi ni hili hapa: -
FT:  Manchester United possession 44% na Chelsea 56%.
Dak ya 32 willian anawaandikia Chelsea bao safi sana na kumfanya David De Gea kuchukia vile defenders wake waliacha gap kizembe na kusababisha kuwa nyuma kwa goli moja. Lakini dak 7 baadae yaani dak ya 39 zilipigwa pasi ndani ya 18 ya Chelsea na hadi kuwafanya watu wasahau kuwa hiyo ni man United. Pasi iliyomkuta Anthony Martial aliyeipeleka kwa Lukaku naye akajikuta akimtazama Courtois na huku defenders was Chelsea wakiwa wameduwaa basi akatazama kushoto kwa Courtois lakini mpira akaujaza kulia kwake yaani macho ku mchuzi mkono ku ubwabwa na kusawazisha yaani ikawa 1-1. Hiyo ilienda hadi mwisho first half.

Kipindi cha pili kilishuhudiwa Martial akitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Jesse Lingard.  Alionekana Lukaku akiwa upande wa kulia aliyeachia krosi safi sana iliyomkuta Lingard aliyechumpa na kuukwamisha mpira kwenye nyavu za Courtois na kuandikia United bao la 2 na la ushindi.

Kwa ushindi huu unaifanya United kurudia nafasi yake ya 2 iliyoshikwa na Liverpool kwa chini ya saa 20.

Mourinho na Conte walikuwa watulivu sana leo wakinong'onezana jambo na kucheka na mwisho wa game wakipeana mikono bila shida yoyote.

Baada ya goli la 2 muda flani Sanchez alitolewa na akaingia Eric Bailly huku akibeba kikaratasi chenye ujumbe toka kwa Mourinho kwenda kwa Nemanja Matic. Inasemekana alimwambia kueneza habari kwa wenzake kuwa goli 2 zatosha na kwa sababu muda unayoyoma basi wapaki basi tu yatosha.

Kijana Mctominay ameonekana kupevuka kisoka hasa kwenye mechi kubwa. Ameonekana Leo akifanya kazi ambayo wengi walitarajia ingefanywa na Herrera ambaye ni majeruhi. Vyombo kadhaa vya habari jana na leo vilimwita he is too young lakini kawaonesha he is too young kwa kuzaliwa tu bali kisoka he is mastering it.

Lukaku kawa man of the match kwa kazi nzuri ya kunyamazisha watu aka haters wake kwa kuifunga his former club na kutoa assist kwa his teammate Lingard.

Pogba alikuwa anathema kama anawatania Chelsea kwani alifanya vitu jinsi alivyotaka yeye. He is a big man.

#AbelRKayUpdate

Comments

Popular posts from this blog

MAKUNDI CHAMPIONS LEAGUE NA SHIRIKISHO AFRIKA

Yanga Sc kundi A Klabu Bingwa Afrika na Simba Sc kundi A Shirikisho Afrika. Hapo chini ndio mpangilio wa makundi na timu zake. Je, nani kati ya timu zetu za bongo atatoboa kwenda robo fainali? Weka maoni yako kwenye komenti tafadhali.

Hawa Ndiyo Real Madrid Waliowafunga Man City Champions League Jana Usiku

Man City wakiwa wanaongo za kwa 2-1 dhidi ya Real Madrid huku zikiwa zimebaki dakika si zaidi  ya tatu walionekana kama ingekuwa ni timu ya tatu ya Uingereza kuifunga Madrid kwenye uwanja wa Bernabeu. Lakini vijana hao wa Mancini badala ya kuinza kampeni yao kwa ushindi walijikuta wakiachwa nyuma na kuwaangalia Madrid wakiibuka na ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha na kisha Cristiano Ronaldo kufunga goli la tatu na la ushindi, goli lililomfanya bosi wao Jose Mourinho kuslide uwanjani akishangilia goli hilo na Ronaldo. This was the real happiness now from Ronaldo BBC football pundit Robbie Savage alikuwa uwanjani huku Bernabeu. (quoting from BBC SPORTS) "Maicon was not at the races at all in the first half at right-back. He was a passenger and it was like City were playing with 10 men. Cristiano Ronaldo kept coming inside him. "In the second-half, Vincent Kompany looked at what was happening and came across to that wing more. Ronaldo did not...