Magoli yaliyofungwa na Romelu Lukaku na Alexis Sanchez yalitosha kuizamisha Huddersfield walipowatembelea Manchester United Old Trafford Jana Jumamosi katika mchezo uliochezwa saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kichapo hicho walichotoa United ni kama kisasi kwani katika mzunguko wa kwanza walizimwa kwa 2-1 na Huddersfield. Japo mbali na kichapo ushindi huo umekuwa muhimu sana kwao kwani unawahakikishia kubaki nafasi ya pili na kupunguza umbali au utofauti wa alama kati yao na vinara wa ligi msimu huu Manchester City ambapo sasa kuna tofauti ya alama 13 kati yao.
Lukaku alifungua matumaini ya ushindi jana baada ya kuunganisha krosi safi iliyopigwa na Juan Mata kunako dakika ya 58 kipindi cha pili. Kunako dakika ya 68 Alexis Sanchez aliangushwa ndani ya 18 za Huddersfield na refa kuamuru ipigwe penati. Sanchez alipiga penati hiyo lakini kipa wa Huddersfield aliiona na kuicheza na kwa bahati mbaya kwake na nzuri kwa Sanchez ilimrudia na kuuweka mpira nyavuni na kuandika goli la pili kwa United.
Sanchez alikuwa na mchango mkubwa sana katika ushindi wa United jana hasa kipindi cha pili. Alionekana akicheza kwa nguvu zote, akitumia akili nyingi na alijikuta akichezewa madhambi mara nyingi sana kuliko mchezaji yeyote jana. Hata Juan Mata alipata mpira toka kwa Sanchez kabla hajapiga krosi iliyomkuta Lukaku.
Kwenye kipindi cha kwanza ilionekana United walistahili kuzawadiwa penati baada ya McTominay kuchezewa madhambi mabaya sana lakini refa alikataa kutoa penati badala yake ikageuka kuwa fair play.
Juan Mata aliibuka kuwa man of the match kutokana na mchango wake mkubwa kwenye mchezo huo na kwa jinsi alivyokuwa imara sana kwenye eneo la kiungo na kuunganisha wengine kimchezo.
Pogba, Rashford na Martial waliingia kipindi cha pili baada ya Lukaku, Lingard na Mata kupumzishwa.
Jumapili ijayo Manchester United watawatembela Newcastle United.
Comments