Alaa Kumbe!!! WACHEZAJI WA CHELSEA WALICHUKIA KITENDO CHA KOCHA WAO KUMFWATA NA KUMKUMBATIA LIONEL MESSI
Alaa!!! Kumbe!!! WACHEZAJI WA CHELSEA WALICHUKIA KITENDO CHA KOCHA WAO KUMFWATA NA KUMKUMBATIA LIONEL MESSI.
Habari zimevuja kuwa ile siku ambayo Chelsea walifurumushwa kwa aibu nje ya mashindano ya champions League kwenye hatua ya 16 bora, kocha wa Chelsea, Antonio Conte aliwaudhi vibaya sana wachezaji wake. Kivipi?
Baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa, Antonio Conte alienda na kumfwata Lionel Messi na kumpongeza kwa soka lake matata na mahiri na kisha kumkumbatia. Kama hiyo haikutosha, Conte alirudi tena mara ya pili na kuzungumza na Messi. Dah basi kitendo hichi kiliwaudhi saaana wachezaji wake.
Conte mwenyewe alisema kuwa ni vizuri na inapendeza kumpa pongeza kwani alistahili kwa soka aliloonesha.
Kwa kukukumbusha tu, Lionel Messi alifunga mabao mawili siku hiyo huku yote yakipita katikati ya miguu ya Thibaut Courtois aka doba na huku akitoa msaada (assist) kwa goli la Ousmane Dembele.
Haya bhana hayo ni ya Chelsea Football Club.
Comments