Alvaro Morata atupwa nje ya kikosi cha Spain
Katika maandalizi ya mashindano ya kombe la dunia kocha Spain ameamua kumuacha nje ya kikosi Alvaro Morata kutokana nakutokuwa kwenye fomu nzuri huku ikijulikana kuwa mara ya mwisho tangu afunge goli ilikuwa boxing Day mwaka jana. Pia mchezaji huyo amesumbuliwa na majeraha mara kadhaa. Wakati huo anapata wakati mgumu kudumu kwenye kikosi cha kwanza tangu ujio wa Olivier Giroud.
Spain wanatarajiwa kupambana na Ujerumani na Argentina kwenye mechi za kirafiki kujiandaa na fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Urusi kuanzia Juni 14 mwaka huu
Comments