Arsenal wawamiminia Watford FC risasi za kutosha
Katika mchezo wa premier League uliochezwa leo jioni Arsenal wamewabugiza Watford bila huruma kwa kuwachabanga magoli 3-0. Magoli yao yalifungwa na Mustafi, Aubameyang na Mkhitaryan. Ushindi huu ni kama kisasi kwao kwani kwenye mzunguko wa kwanza Watford walinyanyasa Arsenal na kuondoka na point zote.
Ushindi huu pia umekuja baada tu ya kushinda mchezo wao dhidi ya AC Milan kwenye mashindano ya UEFA Europa League lakini kabla ya hapo walishapoteza mechi 3 mfululizo zikiwemo 2 za premier League na moja ikiwa ni fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City.
Comments