CR7 AWATAKA REAL MADRID WAMSAJILI MO SALAH NA SIO HAZARD
Inasemekana Cristiano Ronaldo anavutiwa Sana na mshambuliaji wa Liverpool na kwamba anataka uongozi wa Real Madrid waache mpango wao wa kutaka kumsajili Eden Hazard wa Chelsea na badala yake wamsajili Mohamed Salah kama sio kipindi hiki cha majira ya joto basi msimu ujao.
Eden Hazard amekuwa akikosolewa mara kadhaa juu ya ubora wake kwani hajakaa katika huo ubora kwa muda wa kutosha kuweza kishawishi mashabiki wa soka. Pia wengi wanasubiri ujio wa kombe la dunia ili waone ubora wake haswa pale atakapoipigania nchi yake ya Ubelgiji ili basi aweze kufunga vinywa vya wanaomkosoa kuhusu kiwango chake.
#AbelRKayUpDates
Comments