FT: BRIGHTON Brighton & Hove Albion FC 2, Arsenal 1. JAHAZI LA ARSENAL LAZAMA TENA. MASKINI WENGER.... MASHABIKI WASEMA "WENGER OUT! "
Mzee Wenger amekula kichapo kingine leo toka kwa vijana wa Brighton Hove cha 2-1 katika mchezo wa premier League.
Wiki iliyopita Arsenal walikutana na Manchester City Mara mbili kwenye EFL CUP na Premier League na kupewa kichapo cha 3-0 kwenye kila mechi.
Baadhi ya mashabiki walionekana leo uwanjani wakinyanyua bango lililosomeka, "Wenger out" Wakimaanisha kuwa wamechoshwa na vichapo mfululizo hivyo kocha hana budi kuondoka.
Comments