FT: TAIFA STARS 2, DRC THE LEOPOLDS 0
TAIFA stars leo wamewatoa watanzania kimasomaso baada ya kuwaadabisha The LEOPOLDS DRC kwa kuwaburuza kwa magoli 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa kwenye dimba la Taifa jioni leo.
Hadi kipindi cha kwanza kinaisha hakukuwa na timu yoyote iliyoona lango la mwenzake. Lakini kunako kipindi cha pili timu zote mbili zikicheza mpira wa umakini zaidi huku zikiviziana na kushambuliana kwa zamu ilishuhudiwa Mbwana Samatta akiandika bao la kwanza kwa Stars na huku dakika zikiyoyoma Shiza Kichuya akaipatia Stars goli la pili.
Naweza kusema leo Stars wamecheza mpira wa kujituma na kujiamini na wenye akili na usikivu toka kwa kocha wao huku Yondani, Nyoni na Gadiel wakiongoza safu ya ulinzi yenye umakini sana; na Samatta, Kichuya na Simon Msuva wakiisumbua vibaya sana lango la wakongoman.
Kabla mechi ya leo, Stars walipambana na Algeria na kuambulia kipigo cha 4-1 wakiwa ugenini.
#Hongera #TaifaStars
Comments