BAADA YA LIVERPOOL KUPANGWA NA MANCHESTER CITY KWENYE ROBO FAINALI YA UCL, JE, KLOPP AMESEMAJE?
Jurgen Klopp, kocha wa Liverpool amefunguka kuhusiana na timu yake kupangwa kupambana na Manchester City kwenye robo fainali ya UCL.
Amesema, "Nilishasema awali na bado ni ukweli, siku zote ni Hawaiian kwenye droo kwamba utapangiwa jirani yako, lakini kusema ukweli mimi wala sijali kabisa, nikama ilivyokuwa awali tu. Tutapambana na tuliyepangiwa ambaye ni Manchester city. Twende kazi.
Tumepoteza mara moja na kushinda mara moja dhidi yao kwenye ligi. Na sidhani kama kabla ya droo wangepangiwa Liverpool.
Labda sisi sio timu nzuri kwenye 8 Bora lakini katika 8 Bora hakunaga mbabe labda timu mbili tu Barcelona na Bayern Munich lakini asente Mungu huu ni mpira na hakuna matokeo kabla ya mechi.
Tuna mechi chache za kucheza hadi huo muda ufike lakini tunasubiria na tutajitoa kwa nguvu zote.
Haya hayo ni ya Klopp tusubiri kwa Guardiola atasemaje.
Comments