Kumbe Eden Hazard alichezeshwa namba 9 ya Uongo dhidi ya Man City!!!!! 😱😱😱
Eden Hazard wa Chelsea amelalamika na kulaumu mbinu iliyotumika katika mchezo wao dhidi ya Manchester City wa premier League ambapo timu yake walikula kichapo cha 1-0 pale Etihad Stadium jana Jumapili.
Amedai kwamba kocha wake alimchezesha namba tisa ya uongo ili kuwazuga Man city na yeye mwenyewe hadi sasa hajui kwa nini ilikuwa hivyo. Pia aliongeza kuwa haikuwa rahisi kwao kupambana dhidi ya vinara hao wa ligi kwani hawakuwa hata na uwezo wa kumiliki mpira ili waweze kufanya mashambulizi huku yeye mwenyewe akishuhudiwa kugusa mpira mara chache sana kitu ambacho sio kawaida kwake.
Pia ilishuhudiwa Chelsea wakishindwa kabisa kupiga shuti hata moja lililolenga lango la wapinzani yaani shoot on target.
Comments