Marouane Fellaini: Mimi sio mchezaji mkorofi wa mtukutu. I'm not an aggressive player, says Marouane Fellaini.
Kiungo wa Manchester United Marouane Fellaini amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye sio mchezaji mkorofi wala mtukutu awapo uwanjani. Amedai kuwa kazi yake yeye awapo uwanjani ni kuhakikisha kuwa anaunasa mpira uliopotea na kuurudisha kwenye imaya yao na ndio maana huwa anapata maonyo ya yellow kadi mara kadhaa. Amesema kuwa wengi hudhani kuwa yeye ni muhuni kutokana na style ya uchezaji wake jambo ambalo sivyo.
Comments