Mourinho happy for the referee not to send off Klopp. Mourinho Aridhishwa na kitendo cha refa kutompa adhabu Klopp kwa kutoka nje ya eneo lake.
Katika mchezo uliopigwa Jumamosi Manchester United vs Liverpool FC, kocha Jurgen Klopp alikasirishwa na ukabaji wa beki wake Lovren na hivyo kuanza kufoka kwa hasira na kujikuta ametoka nje ya eneo lake. Kitendo hicho kilisababisha refa amwendee na kuzungumza nae ili kumtuliza lakini hakumpa adhabu ya kutoka kwenye bench.
Kocha wa Manchester United akihojiwa na vyombo vya habari alisema kuwa japo wasingeamini lakini yeye alifurahishwa na refa kutomtoa Klopp kwenye benchi. Mou aliongeza kusema kuwa jambo kama hilo lilimtokea yeye kwenye mechi kati ya crystal Palace na Manchester United pale beki wake alipofanya ndivyo sivyo alimfokea na bila kujua akajikuta ametoka nje ya eneo lake lakini refa hakumpa adhabu zaidi ya kuzungumza nae tu juu ya kosa hilo.
Comments