Arsenal na Atletico Madrid Watoshana Nguvu Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Europa League: Lacazette 1, Griezmann 1.
Hajatokea mbabe katika mchezo wa Arsenal dhidi ya Atletico Madrid uliopigwa jana usiku. Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza katika michezo miwili ya nusu fainali ya Europa League.
Alikuwa ni Lacazette aliyowapatia Arsenal matumaini baada ya kupachika bao kunako dakika ya 61 na kuamsha shamrashamra kwa mashabiki wa Arsenal waliofurika uwanjani kushuhudia timu yao na kuona kama itawapatia matumaini ya kutinga fainali na hata kutwaa ubingwa wa Europa.
Lakini matumaini ya Arsenal yakaingia mashakani mara baada ya Griezmann kusawazisha bao kunako dakika ya 82. Atletico hao pia walipata pigo mapema sana baada ya mchezaji wao mmoja kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 10 na kuwafanya kucheza wakiwa 10 uwanjani kwa takribani dakika 80.
Picha zaidi za mechi

Comments