Kiungo wa Manchester United ameonesha dhahiri kuwa yupo tayari kuondoka Old Trafford akiwa amemaliza mkataba wake.
Imeripotiwa kuwa mwezi uliopita alishakutana mara tatu na bosi wake José Mourinho na akapewa dau la mshahara wa pauni 140,000 lakini aligoma. Mshahara wake kwa sasa ni pauni 80,000 kwa wiki. Fellaini amesema kuwa wakati wake wa kuwa Old Trafford umefika kikomo na sasa ni bora aondoke.
Club kadhaa ulaya zinamuwania Fellaini zikiwemo, Juventus, PSG, West Ham, Leicester City, nk na ameona ni bora aondoke kwani pamoja na kubadilisha mazingira lakini atapata faida ya kuweka kibindoni mshaharakwa wiki mara mbili ya anaopata sasa.
Comments