Kwa mara nyingine tena Manchester United na Arsenal zitakutana Jumapili hii kwenye awamu ya pili ya mchezo wa premier league.
Mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Old Trafford unatarajiwa kuwa mkali na mzuri kama ilivyokawaida zikutanapo timu hizi mbili. Hasa ikizingatiwa uhasama na upinzani wa hali ya juu uliopo kati ya meneja wa Arsenal, Wenger, na meneja wa Manchester United, Mourinho.
Akihojiwa na vyombo vya habari, Wenger amesema anataka kuondoka kwa amani kwa hivyo anatarajia makaribisho mazuri toka kwa Mourinho na mashabiki wa soka wa Man United pale Old Trafford. Lakini pia aliongeza kuwa kuondoka kwake Arsenal hakuna maana kuwa timu hizi na makocha hawa hawatakutana tena kwani tayari amepata maombi toka timu mbalimbali zikimtaka kukochi kwa hiyo yeye anaondoka Arsenal lakini hastaafu. Pia aliongeza kuwa kwa kifaransa neno goodbye wao husema, 'au revoir' akimaanisha tutaonana tena.
Wenger na Mourinho wamekuwa wapinzani wakubwa kwenye kazi ya ukocha tangu Mourinho alipokuwa Chelsea na sasa yupo Manchester United. Kuna wakati walifikia hata kukamatana utadhani walitaka kupigana makonde. Lakini Wakati huu Mzee Wenger amemwomba Mourinho waweke tofauti zao kando ili yeye aondoke kwa amani.
Comments