Mambo ya usajili yameanza kupamba moto baada ya club ya Manchester United kukamilisha usajili wa kiungo kinda kutoka Slovakia Martin Svidersky.
Svidersky mwenye umri wa miaka 15 amesaini mkataba wa miaka mitatu hadi 2021 na atajiunga na kikosi cha Manchester United cha under 18 kuanzia msimu ujao.
United wamewazidi kete Chelsea, Liverpool, Celtic, Man City, Inter Milan na Borussia Dortmund ambao walikuwa pia wakimwania mchezaji huyo.
Martin Svidersky anaongea lugha tano ambazo ni Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kigiriki, na Kislovakia ambayo ndo lugha ya kwao.
Comments