Paul Pogba Awaomba wenzake kupambana kesho dhidi ya Arsenal
Akiongea katika mahojiano na Skysports, kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesema na kuwataka wenzake kupambana vilivyo dhidi ya Arsenal watakaopambana nao kesho Jumapili dimbani Old Trafford katika mchezo wa premier league.
Katika mechi ya awali mzunguko wa kwanza, Arsenal walifungwa nyumbani kwao kwa 3-1 huku Pogba akitoa assist 2 na badae akitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Pia Pogba ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya wadau wa soka kuwasifia viungo wengine kwenye soka la Uingereza na kumponda yeye.
United wamekuwa wazuri msimu huu na hadi sasa wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya Mahasimu wao wa jadi Manchester City ambao tayari wameshatangazwa mabingwa baada ya kufikisha point ambazo hazitafikiwa na timu yoyote. Hivi karibuni wamecheza na Chelsea, Man City na Spurs na kuzifunga zote huku wakitokea nyuma na kushinda mechi.
Kesho ndio kesho pale Mourinho atakapomkaribisha na kumwaga Wenger. Je uhasama kati yao utaendelea?
Comments