LEVANTE 5-4 BARCELONA: Game yenye hat-trick 2
- Magoli 9 yakitinga nyavuni huku ndoto ya wababe Barcelona kumaliza ligi bila kufungwa ikiyeyuka pamoja na Philippe Coutinho kuweka jitihada na kupiga hat-trick; Lakini Emmanuel Boateng nae akipiga matatu.
- Philippe Coutinho hataisahau kamwe hat-trick yake ya kwanza kwa Barcelona. Alijitahidi zaidi ya wengine kuondoa aibu ya kihistoria akifunga magoli matatu lakini haikusaidia akijikuta yeye na timu yake wageuka jahazi lililozama.
- Lionel Messi aliachwa apumzike na hiyo yaweza kuwa sababu rahisi kuwa kutokuwepo kwake kuliigharimu Barcelona.
Brings You Global News!
Comments