Neymar Jr Kwenda Manchester United au Real Madrid Msimu Ujao
Mshambuliaji wa PSG Neymar Jr amezungumzia mstakabali wake kwa msimu ujao na inawezekana akapata wakati mgumu kuchagua ka?a aende Manchester United ama Real Madrid.
Neymar aliyehamia PSG akitokea Barcelona alishajutia kukurupuka kwake na kwenda Ufaransa ambako aliona soka la kule sio mahali pake na siyo kiwango chake akitaja kuwa halina ushindani wa kutosha.
Manchester United na Real Madrid ndio timu ambazo zimeonesha nia kubwa ya kumtaka Neymar, huku kila mojawapo ikitaka kufanya hivyo kwa lengo la kuimarisha kikosi chake kwani imeonekana wazi wapinzani wao kwenye ligi zao wamejidhatiti vizuri mno. Manchester United wakimaliza ligi kwenye nafasi ya pili nyuma ya mabingwa wapya Mahasimu wao wa jadi Manchester City kwa tofauti ya pointi 19, na kwa upande wa Madrid wakishindwa kabisa kutamba mbele ya wapinzani wao wakuu Barcelona na kuwaacha wakitwaa ubingwa wa La Liga.
Kwa mtazamo wako kama mpenzi wa soka, ungependa Neymar Jr aende wapi kati ya Manchester United na Real Madrid?
Comments