Yaya Toure: Naweza kwenda Man United
Pamoja na kuichezea Manchester City kwa takribani miaka nane, kiungo wa Man City, Yaya Toure amesema angeweza kufikiria kuhamia Manchester united iwapo nafasi hiyo itatokea.
Toure anaondoka City baada ya kwisha kwa msimu wa 2017-2018, na bado haijajulikana ataelekea wapi.
"Ningependa kwenda mahali ambako nitashinda na kupata mafanikio. Itakuwa vigumu kwangu siku moja kucheza dhidi ya City, lakini sina budi kufanya hivyo kwa ni sehemu ya maisha yangu.
"Nimekuwa nikicheza mpira kwa muda mrefu, siwezi kufanya kazi za ofisini au kingine chochote, nijuacho Mimi ni mpira.
"Kujiona katika club nyingine kwangu itakuwa ngumu. Nimekuwa sehemu ya City kwa muda mrefu. Nataka kusema kuwa nitaendelea kucheza kwenye level ya juu, Uefa au Ueropa league.
"Nataka kucheza kwa miaka miwili zaidi. Lazima iwe kwenye level ya juu halafu ndipo nifanye mambo mengine.
Comments