FIFA WORLD CUP 2018 GROUP D: ARGENTINA WACHARAZWA 3 MZUKA NA CROATIA NA KULIA UWANJANI. SASA WATEGEMEA KUPENYA TUNDU LA SINDANO ILI KUSONGA MBELE
FIFA WORLD CUP 2018 GROUP D: ARGENTINA WACHARAZWA 3 MZUKA NA CROATIA NA KULIA UWANJANI. SASA WATEGEMA KUPENYA TUNDU LA SINDANO ILI KUSONGA MBELE
>Argentina Waadhibiwa 3-0 na Croatia kwenye mechi ya kundi D world cup 2018
>Ni kichapo kikali kwa Argentina katika hatua ya makundi
>Croatia wasonga mbele kwa mara ya kwanza tangu m2aka 1998
Miaka takribani minne wakati Argentina walipopoteza dhidi ya Germany na Germany kutwaa ubingwa wa dunia, maelfu ya Wargentina walivunjika moyo. Sasa kwa kilichotokea kwenye mechi ya jana nadhani kinachoma moto kwenye makovu ya wargentina tena.
Argentina yenye wachezaji wengi wazurina maarufu akiwemo Lionel Messi ilitazamiwa kufanya makubwa hasa kwenye mechi yake ya pili ya hatua ya makundi lakini mambo yakageuka na kuwa vilio kutawala uwanjani utadhani kuna watoto au wanawake wanalia.
Nafasi nyingi walizozikosa katika mashambulizi yao zikigeuka kuwa neema kwa Croatia ambao hawakufanya ajizi kwenye nafasi zao na kuanzia kioindi cha pili ndipo wakaanza kuwabadilikia wapinzani wao na kuanza kuwasulibisha mithili ya jambazi aliyekuwa akisakwa kwa muda mrefu na sasa anapatikana....... kipigo chake hicho sasa!
Siku nne toka sasa ndipo itajulikana kama Argentina wanayaaga mashindano ama la. Na kwa sasa nadhani labda wafanye mazoezi ya kujifunza kupenya kwenye tundu la sindano ndipo waweze kusonga mbele na kama hawataweza kufuzu kupenya tunduni mwa sindano basi wasahau kusonga mbele kwenye mashindano haya ya kombe la dunia.
Argentina were completely outplayed by Croatia na kupewa kichapo kikali cha aibu cha 3 bila.
Wengi humwangalia Lionel Messi na yeye pia analijua hili lakini tatizo linakuja pale matazamio ya wengi yanapofelishwa na timu pinzani ambao hawataki kujali wala kutambua Messi ndio nani.
Vilio vilitawala wakati na baada ya mechi huku shujaa wa soka wa Argentina Diego Maradona akishindwa kuamini kinachotokea uwanjani na kuungana na wachezaji kutoa kilio bila kujizuia ila yeye akililia jukwaani huku wachezaji wakililia uwanjani na vyumbani.
Comments