COMMUNITY SHIELD: MAN CITY 2, CHELSEA 0
Mabingwa watetezi wa Epl, Manchester city jioni ya leo wamewaadabisha vilivyo mithili ya kumchinja kuku mgonjwa asiyeweza hata kujitetea katika mpambano uliotarajiwa ungeleta ushindani wa hali ya juu lakini walaa.
Magoli ya man city yalifungwa na Sergio Aguero kunako dakika za 13, 58. Na hivyo man city kutwaa taji hilo la community shield ambalo ni kiashilio cha ufunguzi wa ligi ya Epl itakayoanza tarehe 10 Ijumaa ya wiki ijayo.
Comments