CR7 UEFA Forward of the Season
Kwenye droo ya leo Alhamisi ya champions league group stage, Cristiano Ronaldo ametunukiwa kuwa mshambuliaji bora wa msimu uliopita wa UEFA.
Ronaldo alikuwa mfungaji bora kwenye mashindano hayo akiwa na magoli 15 huku akiwa mshambuliaji tegemezi wa club yake ya Madrid msimu uliopita.
Magoli yake yaliisaidia Real Madrid kushinda taji la club bingwa ulaya kwa Mara ya tatu mfululizo na la nne ndani ya miaka mitano, huku likiwa ni la tano kwa Ronaldo.
Moja ya goli lake Kali sana alilofunga dhidi ya Juventus likiitwa bicycle kick likitajwa kuwa goli bora la msimu akimshinda mwenzake Gareth Bale aliyefunga la kufanana nalo.
Lionel Messi hakutajwa kabisa kugombea tuzo hii badala yake alikuwa ni Mohamed Salah aliyepata nafasi ya pili huku akiachwa mbali sana na Ronaldo pamoja na kuibeba Liverpool hadi fainali za champions league.
Ronaldo sasa ameachana na Madrid na amejiunga na Juventus huku akiwa na matumaini ya kuwndeleza ushindi.
Comments