"José Mourinho ni bora apige kimya tu." - Sven-Goran Eriksson
Aliyewahi kuwa meneja wa kikosi cha taifa cha England Sven-Goran Eriksson anaamini kuwa meneja wa Manchester United, José Mourinho anakosea pale anapojibu shutuma au hukumu toka vyombo vya habari, na kwamba ingefaa abakie kimya.
Msweden huyo siyo mgeni kwenye hukumu, shutuma za vyombo vya habari vya England kwa sababu aliwahi kukutana na adha kama hizo wakati alipokuwa kocha wa England kwa takribani miaka minne.
José Mourinho amekutyana na adha kama hizo katika miaka yake ya ukocha kwenye premier league na inaonekana kwamba mambo yamekuwa mabaya zaidi baada ya Mourinho kuondoka kwenye kikao na wanahabari baada ya timu yake Man United kubugizwa bila huruma wala aibu kwa 3-0 wakiwa nyumbani Old Trafford mechi iliyopigwa usiku wa jumatatu iliyopita.
"Siku zote mambo yako hivyo, unapokosolewa kama kocha ni bora ukae kimya" alisema Sven-Goran Eriksson akiliambia 'Sky Sport'
"Usijaribu kujitetea kwa sababu matokeo yatakutetea, utajitetea kwa matokeo ya mchezo. Ukisoma kilichoandikwa gazetini, usijibu.
Hasa pale unapoanza kubisha na wanahabari kamwe huwezi kuwashinda. Siku zote utapoteza tu kwa sababu wanahabari ndio waamuzi, wao ni waandishi. Hivyo kaa kimya, imamisha kichwa chako, endelea kuchapa kazi na waoneshe watu kuwa katika mechi ijayo itacheza mpira mzuri na utashinda."
Lakini Mourinho haonekani kuchua ushauri kama huo wa Eriksson kwa sababu hasira zake zinaonekana kuzidi kichwa pale anapotokea kukosolewa hasa na wanahabari.
#AbelRKayUpdates
Comments