MAN UNITED BADO WANAWAZA DEAL LA KU SWAP MARTIAL NA WILLIAN
Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka leo jumapili asubuhi, Manchester United wanaweza kujaribu kuwashawishi Chelsea kubadilishana wachezaji, Martial kwa Willian.
Willian amekuwa akiendelea kuhusishwa na kuihama Chelsea kipindi hili cha kiangazi, wakati mahusiano ya Martial na José Mourinho yakiwa sio mazuri kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror kila timu imeweka gharama inayofanana ya mchezaji wake ikiwa ni kiasi cha pauni milioni 75, hii ikimaanisha kwamba ubadilishanaji wa wachezaji hawa unaweza kutokea.
Walakini, baada ya uhamisho wa Kwenda Barcelona kushindikana, willian amedai kuwa yeye bado anafurahia kubaki Chelsea. Na huku bosi mpya wa Chelsea Maurizio Sarri akiwa yuko tayari kufanya kazi na mbrazil huyo na anaweza kumpatia muda wa kucheza michezo mingi zaidi ikilinganishwa na alivyuofanya Antonio Conte.
Wachezaji hawa wawili wote waliwakorofisha mabosi wa baada ya willian kuchelewa kujiunga na timu baada ya kombe la dunia kwa madai ya paspoti kuisha muda wake wakati Martial aliondoka Marekani ilikokuwa timu katika tour na Kwenda kushuhudia kuzaliwa kwa mtoto wake huku akidai, familia ni ya kwanza kwake.
Comments