Mourinho Anaamini Kuwa Pereira Sasa Yupo Tayari Kupambania Namba at Old Trafford
Mourinho amefunguka na kusema kuwa kwa sasa Pereira wamepata nguvu ya kiakili kwa ajili ya kupambania position kwenye kikosi cha Man United.
Kiungo huyo wa miaka 22 ameshacheza kwenye mechi zote mbili za premier league za United na tayari ameitwa kwenye kikosi cha Brazil kwa Mara ya kwanza kwa ajili ya mashindano ya UEFA Nations League dhidi ya USA na El Salvador.
Boss huyo wa United ameweka wazi kuwa kwa Pereira kucheza misimu miwili nchini Hispania akiwa Granada na Valencia kwa mkopo kumemsaidia sana kujijenga kiakili kisoka.
"Sikufurahia kwa kutokucheza kwenye namba yake alipokuwa Valencia", Mourinho alisema.
" Lakini na maono ya kibinadamu ilimsaidia sana kupata ujuzi, amekuwa mwanaume sasa na ana utayari kiakili na kimwili."
"Halafu likaja swala la Premier league Kumchezesha nafasi ambao tunadhani inamfaa zaidi, kumwelimisha na kumfanya aielewe nafasi yake."
"Kutokana na ukweli kwamba tulikuwa na viungo watatu pekee kwenye mechi za preseason ilimfanya acheze mechi zote kwa dakika 90, kitu ambacho kilikuwa kizuri sana kwake."
Ingawaje alicheza mechi zote mbili za premier league, lakini alipumzishwa Mara baada ya kipindi cha kwanza kwisha walipokutana na Brighton wiki iliyopita. Pia anaweza kupata nafasi nyingine pale United watakapokutana na Spurs Jumatatu usiku dimbani Old Trafford.
Comments