WILLIAN AFUNGUKA KUHUSU ANTONIO CONTE
"Ningekuwepo Chelsea bado kama Conte Asingeondoka? La hasha" Afunguka Willian
Kama Antonio conte angesalia kama meneja wa Chelsea, mbrazil anayekipiga chelsea, Willian amefunguka na kusema kwamba yeye angeondoka Stamford Bridge.
Willian anasema kuwa asingeweza kubakia klabuni hapo kama Antonio Conte angebakia kuwa meneja.
Nafasi ya Conte ilichukuliwa na muitalian mwenzake Maurizio Sarri huku akiwa in charge ameshuhudia timu yake ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Huddersfield kwenye mechi yao ya ufunguzi ya EPL iliyopigwa Jumapili ya jana.
Comments