Willian Agusia muungano wake na Mourinho
José Mourinho na willian wameshashinda premier league wakiwa Chelsea, huku mbrazil huyo akiwa yuko tayari kufanya kazi kwa Mara nyingine na bosi wake huyo wa zamani.
Winga wa Chelsea, Willian amegusia kuwa angekuwa tayari kusaini Manchester United kwa kusema kuwa anataka kufanya kazi tena na José Mourinho.
Willian na Mourinho wameshinda Epl Mara mbili wakiwa pamoja pale Stamford bridge and willian amekuwa akihusishwa Kwenda old Trafford.
Mourinho anatamani sana kuimarisha safu yake ya ushambuliaji huku kukiwa kumebakia siku chache tu kwisha kwa dirisha la usajili hapo Alhamisi 9 Agosti.
Willian pia amesema kuwa angefurahia kubakia Chelsea kwa msimu wa 2018-2019 lakini pia ameacha mlango wazi endapo uwezekano wa kuungana na Mourinho utakuwepo.
"Mourinho ni meneja mzuri ambaye haijawahi kutokea Mimi kufanya nae kazi. Tuna mahusiano mazuri nasi ni marafiki." Willian aliliambia ESPN Mbrazil baada ya Chelsea kula kipondo cha 2-0 toka kwa Manchester City kwenye Community Shield.
"Wakati mwingine tunaongea, tuna text, tunatumiana meseji kupitia WhatsApp. Ni meneja mzuri sana. Nilifurahia sana kufanya nae kazi. Natumaini nitaweza kufanya nae kazi tena siku moja. " Aliongeza Willian.
Comments