KIPA wa Yanga Klaus Kindoki Aomba Radhi
Kipa wa Yanga Mkongoman Klaus Kimdoki, amewaomba radhi mashabiki na wanachama wa timu hiyo kufuatia kufanya makosa ama uzembe uliosababisha Stand United kupata magoli matatu kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Baraa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar, Yanga iliahimda mabao manne kwa matatu huku Stand United ikifunga mabao hayo yaliyotokana kwa sehemu kuwa na uzembe wa Kindoki.
Kindoki alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Racing de Kinshasa, alinena lawama toka kwa mashabiki wa Yanga kutokana na kuonesha kiwango dhaifu kwenye mpambano huo.
Akizungumza na gazeti moja wapo jijini Dar, Kindoki alikiri kufanya makosa ambayo yaliwagharimu lakini akasema amejifunza kutokana na makosa hayo na kamwe hayatajirudia tena kwenye mechi zijazo.
"Ni kweli nimekosea na ninajutia lakini napaswa kusamehewa na kupewa nafasi kwa sababu nimejua kosa langu na ninaamini halitojirudia tena. Kitu cha msingi naomba mashabiki waendelee kuwa na imani nami na wasahau yaliyotokea." Alisema Kindoki.
Comments