#LondonDerby: #Epl: #Sarriball style yadoda Wembley!
Tottenham 3-1 Chelsea: Magoli ya Dele Alli, Harry Kane na Son yaharibu mpango wa Chelsea wa kutofungwa!
Kutofungwa kwa Chelsea katika epl kumeingia doa baya lisilotakata hata kwa sabuni gani baada ya mchezo mzuri wa kuvutia wa Tottenham katika dimba la Wembley uliohakikisha mashabiki wa Chelsea wanalizwa machozi ya damu kwa kuwekwa magoli mara 3.
Dele Alli akifungua ukurasa wa magoli kwa wenyeji baada ya dakika 7 tu za mchezo huku kichwa chake kikipeleka mpira kwenye post ya mbali sana, aka anakotagia kanga.
Harry Kane akaongeza la pili akiichungulia kona ya chini baada ya mabeki wa Chelsea kumwachia apige shuti la mbali.
Son akafanya magoli kuwa 3 kwa Spurs mapema kunako kipindi cha pili baada ya mkorea huyo kufanya kitu kinaitwa kwa kizungu sensational solo goal.
Olivier Giroud akaingia kutokea bench na kufunga goli la kufutia machozi kwa wageni Chelsea.
Comments