Klabu ya Real Madrid inatarajia kumtangaza Santiago Solari kuwa kocha wa klabu hiyo mpaka mwisho wa msimu huu baada ya kuiongoza Madrid kwenye michezo minne akiwa kama kocha msaidizi.
Solari ameshinda michezo yote minne aliyoiongoza Real Madrid na kufanya raisi wa Real Madrid Florentino Perez kumwamini na kumpa kazi hiyo.
Awali Real Madrid walitaka kumpa nafasi hiyo kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte lakini dili hilo lilivunjika hatua za mwisho baada ya kushindwa kuelewana huku Conte akidai sababu ni kwamba alitaka kuchukua timu mwezi June na sio katikati ya msimu.
Source: #kwetusport
Comments