Arjen Robben Astaafu Soka
Baada ya kushinda kombe la ligi ya Ujerumani Bundesliga mara 8, winga Arjen Robben ametangaza kustaafu Soka.
Star huyo wa Bayern Munich na Uholanzi amefikia uamuzi huo akiwa na umri wa miaka 35.
Winga huyo amecheza soka lake kwa miaka 19, akiziwakilisha baadhi ya timu kubwa na maarufu ulaya kama PSV Eindhoven, Chelsea na Real Madrid kabla ya kutimkia Bayern Munich mwaka 2009. Amekaa na Bavarians kwa miaka 10 akishinda Bundesliga mara 8 na kufunga magoli 144 likiwemo la ushindi wao dhidi ya Borussia Dortmund kwenye fainali za ligi ya mabingwa ulaya.
Robben ameichezea timu yake ya taifa Uholanzi mechi 96 akifunga magoli 37.
Comments